ludewa

WAISHUKURU SERIKALI KUFUNGUA MIPAKA
na chrispin kalinga.


wananchi  wilayani ludewa mkoani  njombe wameishukuru serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kufungua mipaka ya uuzwaji wa mahindi nje ya nchi na kuwaletea wanunuzi ndani ya mkoa.

wakulima wa mkoani hapo wamesema kuwa bei ya mahindi ilikuwa ni ya chini sana ukilinganishwa na ghalima za pembejeo za kilimo na kwa sasa angalau wamepata auheni ya kuendelea kulima na wesema kuwa wanawaomba wakulima wote wa ludewa licha ya kupata wanunuzi wanawaomba wote wauze kwa bei moja.

hali kadhalika wakulima hao wemesema kuwa wanaomba uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo  kuwasimamia wakulima hao kwa uuzwaji wa mahindi haswa kwa upande wa bei kwasababu baadhi ya wakulima wengine wanauza bei ya hasara wakijua ununuzi hamna.

aidha mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya ya ludewa Ludigija ndatwa amezungumza na kituo chetu cha habari kuwa uamuzi wa wa waziri kufungua mipaka utaleta manufaa makubwa kwa wakulima haswa kwa wakulima wa ludewa kwa kuwa wengi wao wana mahindi mengi na amewataka wakulima wa mahindi kuchangamkia furusa hii na amezungumza kwa licha ya soko hulia kupatikana anawaomba wakulima kuuza bei angalau zaidi ya ile iliyo kuwepo.


hata hivyo waziri wa kilimo amesema kuwa wanunuzi wa mahindiwameelekezwa kwenye mikoa miwili mikoa ya njombe na ruvuma na amesema kuwa baadaye wataelekezwa kwenye mkoa wa songwe sambamba na hilo kiongozi huyo amesema kuwa  wamebaini kuwa maindi yaliyoko nchini ni mengi sana na amesema kuwa anawaruhusu wafanya biashara kupeleka mahindi nnje ya nchi.

pia kiongozi huyo amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuacha maramoja tabia ya kuzuia mazao kutoka kwenye mkoa mmoja kwenda mkoamwingine na wilaya moja kwenda wilaya nyingine.

 .........................../........................................


Maoni